EWURA:Bei mpya ya mafuta kuanza kesho

*Bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 321 kwa lita sawa na asilimia 21.45 mtawalia

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imsema kuwa, bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitaanza kutumika kuanzia kesho Aprili 6,2022 nchini.
Hayo yamesemwa leo Aprili 5, 2022 na Mkurugenzi wa Petroli nchini,Bw.Gerald Maganga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mhandisi Geoffrey Chibulunje

Bw. Maganga amesema kuwa,bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Machi 2,2022.

Amesema kuwa, Aprili,2022 bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 321 kwa lita sawa na asilimia 21.45 mtawalia.

Maganga amesema,toleo lililopita bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 320.33 kwa lita sawa na asilimia 13.29, shilingi 288.50 kwa lita sawa na asilimia 12.69 na shilingi 472.41 kwa lita sawa na asilimia 22.72 mtawalia.

Akizungumzia mwezi Aprili,2022 Bw. Maganga amesema, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini ikihusisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa Machi 2,2022.

"Kwa mwezi Machi, mwaka huu,Bandari ya Mtwara imepokea mafuta ya dizeli tu, hivyo kwa Aprili 2022 bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli kwa mikoa ya Kusini yaani Lindi na Ruvuma zitakuwa sawa na zile zilizotangazwa Machi 2,2022,"amesema Bw.Maganga.

Akizungumzia kwa upande wa dizeli kwa mwezi Aprili, 2022, Bw. Maganga amesema kuwa, bei za rejareja na jumla za dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la mwezi uliopita,bei ya rejareja ya dizeli imeongeza kwa shilingi 281 kwa lita sawa na asilimia 11.12 na bei ya jumla ya dizeli ikiwa imeongeza kwa shilingi 279.99 kwa lita sawa na asilimia 11.67.

Bw.Maganga amefafanua kuwa,hakuna matenki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka Bandari ya Dar es Salaam na kwamba bei za rejareja za mafuta hayo katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

"Mabadiliko haya ya rejareja yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la Dunia, gharama za usafirishaji na thamani ya shilingi ukilinganisha na dola za Marekani,hivyo EWURA inaukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00#,"ameeleza Bw.Maganga.

Hata hivyo, Bw.Maganga amesema kuwa, kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo zisivuke bei kikomo au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na kanuni za EWURA.

Amesema, ni zile zinazopanga bei za mafuta za mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Gazeti la Serikali namba.57 la Januari 28,2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news