IGP Sirro atoa mwezi mmoja kwa makamanda wa polisi

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaagiza Makamanda wa Polisi nchini kote kufanya operesheni ya mwezi mmoja ya kudhibiti makosa ya usalama barabarani ambayo kwa kipindi cha mwezi wa tatu mwaka huu yameonekeana kuongezeka.
IGP amesema hayo kwenye kikao kazi na Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani, Rufiji ma RTOs na DTOs pamoja na Wakuu wa Operesheni kutoka kwenye mikoa hiyo.

Aidha, katika kikao kazi hicho IGP Sirro ametoa agizo kwa wananchi kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuepusha ajali zinazoweza kuepukia.

Katika hatua nyingine, IGP Simon Sirro amekutana na kuzungumza na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Mhe. Hamdi Mansour Abuali aliyemtembelea ofisini kwake Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama na ushirikiano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news