Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Aprili 28,2022

NA GODFREY NNKO

LEO shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.65 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Aprili 28, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Yen ya Japan (JPY) inanunuliwa kwa shilingi 17.86 na kuuzwa kwa shilingi 18.03 huku Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 144.15 na kuuzwa kwa shilingi 145.46.

Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2287.35 na kuuzwa kwa shilingi 2310.22 huku Paundi ya Uingereza (GBP) ikinunuliwa kwa shilingi 2874.05 na kuuzwa kwa shilingi 2903.71.
Aidha,Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2421.16 na kuuzwa kwa shilingi 2445.83 huku Yuan ya China (CNY) ikinunuliwa kwa shilingi 349.03 na kuuzwa kwa shilingi 352.4.

Post a Comment

0 Comments