Waziri Nape atembelea Banda la STAMICO Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO, Happy Mbenyange kuhusu shughuli wanazofanya leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. (Picha na Kadama Malunde 1 blog).
Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira - Kabulo mkoani Mbeya.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiipongeza STAMICO kwa shughuli wanazofanya alipotembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'. Kulia ni Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news