Mheshimiwa Masanja:Vyombo vya habari msipotoshe kuhusu Ngorongoro

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii katika Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro uliofanyika leo Juni 21,2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema kuwa Serikali imechukua jukumu la kukata eneo la Loliondo SQM 4000 ambazo zina usajili na eneo la SQM 2500 likakatwa kwa ajili ya matumizi ya wananchi. 

Masanja amesema kuwa, vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha kuhusu eneo hilo kwa kutaka kuharibu taswira ya wawekezaji nchini Jambo ambalo halina manufaa kwa Taifa.
"Vyombo vya Habari vinapotosha kuhusu mwekezaji aliyepo zaidi ya miaka 30 ambapo kila mwaka vitalu vya eneo Hilo hutangazwa kisheria na kuingizwa katika minada ambapo mwekezaji huyo huibuka mshindi na kupata eneo lake kisheria,"alisema Masanja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news