Ujumbe wa amani Tanzania kuongozwa na Balozi wa Amani Duniani

NA GRACE SEMFUKO-MAELEZO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema, Agosti 23, 2022, Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa ujio wa Balozi wa Amani Duniani na Kiongozi wa kidini kutoka Nchini India Bw. Gurudev Sri Sri Ravi Shankar ambaye atawasili nchini akiwa na ujumbe wa watu 15, na atakuwepo hadi Agosti 27 mwaka huu.
Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 23,2022 wakati akitoa taarifa ya ujio wa Balozi wa Amani

Duniani na Kiongozi wa kidini kutoka Nchini India Bw. Gurudev Sri Sri Ravi Shankar ambaye atawasili nchini akiwa na ujumbe wa watu 15, na atakuwepo hadi Agosti 27 mwaka huu.Amesema pia jioni ya siku hiyo hiyo, Bw. Gurudev anatarajiwa kuendesha Tamasha kubwa la utamaduni katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) na burudani za kiutamaduni za vikundi vya ngoma kutoka Tanzania na India vitatumbuiza ambapo pia atapata fursa ya kutoa mhadhara kwa Watanzania pamoja na kuendesha zoezi la mtindo wa kuvuta pumzi unaoleta furaha na amani.

Mgeni rasmi katika tukio hilo ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Omar Mchengerwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Dkt Abbasi amesema Wizara yake kwa kushirikiana na Ubalozi wa India ndio wanaoratibu ujio huo ambao unalenga kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan za kulitangaza Taifa letu kupitia Royal Tour

Amesema Bw. Gurudev Sri Sri Ravi Shankar ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa kutokana na karama aliyonayo ya kuhuburi amani na upendo, ustawi kwa jamii, kuishi maisha ya furaha, kuepuka migogoro, kuwa na uhuru wa mawazo, na kuona kuwa dunia ni familia ambayo kila mmoja ni wa thamani.

Aidha amebainisha kuwa ujio wa Gurudev ni wa muhimu kwa kuitangaza nchi ya Tanzania kwani kila mahali anapokuwa, hufuatiliwa na mamilioni ya watu duniani kote na pia moja ya mchango wa kipekee kwa dunia anaoutoa ni mbinu imara ya upumiaji inayowezesha ustawi wa kimwili, kiakili, kihisia na kijamii ambapo tayari amebuni kozi 57 za kuifanya jamii Duniani kuwa na tabasamu, kuepukana na msongo wa mawazo na vurugu.

"Katika ziara yake ya Royal Tour nchini Tanzania Bw. Gurudev anatarajiwa kuendesha Tamasha kubwa la utamaduni katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa 11:30 jioni ambapo burudani za kiutamaduni za vikundi vya ngoma kutoka Tanzania na India vitatumbuiza.
 
Bw. Gurudev atapata fursa ya kutoa mhadhara kwa Watanzania pamoja na kuendesha zoezi la mtindo wa kuvuta pumzi unaoleta furaha na Amani.” Amesema Dkt Abbasi.

Nae Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema Uamuzi wa Balozi huyo wa Amani kutembelea nchi ya Tanzania ambayo inatambulika kama kisiwa cha Amani, ni heshima kubwa na kutambuliwa kwa tunu muhimu ya Amani ambayo ni fursa muhimu ya kulitangaza Taifa letu kimataifa na kuongeza chachu ya uhusiano baina ya Tanzania na India ambayo yamedumu kwa muda mrefu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news