Waziri Bashungwa atoa wito kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa kujitoa na kuchangia miradi mbalimbali kwenye maeneo yao.

Mhe.Bashungwa ambaye pia ni Mbunge wa Karagwe mkoani Kagera ametoa wito huo Agosti 20,2022 alipokuwa akizungumza kwenye harambee ya kuchangia wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Ihembe Wilaya Karagwe mkoani Kagera iliyoandaliwa na wananchi kwa ushirikiano wa uongozi wa kata hiyo.

’’Pamoja na malengo ya Serikali ya kila Tarafa iwe Kituo cha Afya, lakini inapotokea wananchi kama nyie wa Kata ya Ihembe mkaamua kuchangia na kuanza kujenga Kituo cha afya, sisi kama Serikali jukumu letu ni kuunga mkono juhudi zenu na kuhakikisha mnakamilisha maelengo yenu,”amesema Mhe.Bashungwa.

Waziri Bashungwa amepongeza wananchi wa Kata hiyo kwa kuonesha mfano na kujitoa kwa michango ya fedha na nguvu kazi ili kuhakikisha wanajenga kituo hicho ambapo hadi sasa wameshachangia zaidi ya sh. milioni 20.

Aidha, Bashungwa ametumia fursa hiyo kueleza mipango mbalimbali ya Serikali ya kupeleka miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, kufikisha umeme katika vijiji vilivyosalia, uboreshaji wa miundombinu ya Barabara na elimu.

Katika harambee hiyo, Mhe.Bashungwa amechangia shilingi milioni 10, Halmashauri imetoa sh.milioni 20 ambapo Jumla ya michango yote iliyopatikana ni Sh.Milioni 32.1.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news