BREAKING NEWS:Bendera ya CHADEMA yazua taharuki ibada ya mazishi kanisani

NA DIRAMAKINI

KANISA la Moravian Ushirika wa Vwawa mkoani Songwe limesitisha kwa muda ibada ya kuwaombea marehemu baada ya mmoja wa marehemu kuwekewa bendera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika sanduku lake wakiwa ndani ya kanisa jambo ambalo kiongozi wa kanisa imemlazimu kutoa mwongozo.

Maelekezo ya Kiongozi wa Kanisa yametolewa kwenye ibada ya kuombea marehemu wawili waliofikishwa kanisani hapo leo Desemba 26, 2022 majira ya saa 6:15 katika makao makuu ya Mkoa wa Songwe-Vwawa.

Katika jeneza la Sarah Shitindi maarufu kama Sarah Miondoko iliwekwa bendera ya CHADEMA jambo ambalo Katibu wa Ushirika huo aliyefahamika kwa jina la Kayuni alilazimika kutoa mwongozo ili ibada iendelee.

Ibada hiyo imeendeshwa na Mchungaji Mwasenga ambapo amesisitiza jamii kuishi ikitambua kuwa, duniani ni wapitaji, hivyo ni muhimu kuacha Dunia safi isiyoharibiwa mazingira yake.

Kutokana na maelekezo ya kuzingatia utaratibu wa kanisa, viongozi wa CHADEMA walitii na kuondoa bendera na ibada ikaendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news