Kajala amtoroka Harmonize tena

NA DIRAMAKINI

HUENDA tayari uhusiano wa msanii maarufu wa Bongo Fleva, Rajab Abdul (Harmonize) na msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja umevunjika.
Ni baada ya saa chache zilizopita, Kajala kupitia ukurasa wake wa Instargram kuchapisha ujumbe ambao unaonesha wazi kuwa, safari ya wawili hao imefikia ukomo,hii ni baada ya tetesi za awali kuenea kwa kasi mitandaoni.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia,ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia😌.

"Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu. Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. I forgive my X and I’m ready for the next.
#Nimekoma#
Temporary post,"imesomeka sehemu ya ujumbe wa Kajala katika ukurasa huo leo Desemba 8, 2022.
Tukio hilo la kushangaza linajiri ikiwa ni miezi kadhaa imetimia baada ya Harmonize kumvalisha pete ya uchumba msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja.

Tukio hilo lilifanyika Jumamosi ya Juni 25,2022 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salam na kulipa jina la ‘Late Lunch’ huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang, Mkurugenzi wa TVE, Francis Ciza ’Majizo’, Aunty Ezekiel, Martin Kadinda na wengineo.

Wawili hao walichumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja na ushee, tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu.

Wakati huo, Kajala alisema: “Hakuna asiyejua tuliyoyapitia, pia mimi si mkamilifu so nikaona kwa nini nisimsamehe, So Harmonize naahidi nitakupenda leo, kesho hadi milele,”.

Aidha, mahusiano ya wawili hayo yalijulikana rasmi Februari mwaka jana, lakini ilipofika Aprili lilisambaratika baada ya kuvuja kwa picha za utupu ambazo Harmonize ilielezwa alimtumia mtoto wa mpenzi wake huyo.

Harmonize akizungumza kabla ya kumvalisha pete Kajala siku hiyo alisema wamepitia mengi na msanii huyo na anashukuru hatua hiyo waliyofikia.

Pia alisema kwa wasiojua yeye na Kajala wamejuana zaidi ya miaka saba iliyopita tangu akiwa hana pa kulala mpaka kupata mafanikio aliyonayo leo.

“Mimi na Kajala tuna historia ndefu ,tulijuana miaka saba iliyopita, nililala kwake nkiwa sina pa kulala mpaka leo mnaponiona hapa,”alisema Harmonize siku hiyo.

Wakati huo huo, Kajala hakuwa si mpenzi tu bali pia ndiye meneja mpya wa mwanamuziki huyo. Pia alikuwa anaongoza timu ya mameneja wa Harmonize akishikilia wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji.

Awali, Meneja wa usanii wa Harmonize Choppa TZ alitangaza habari za uteuzi wa Kajala huku akimkaribisha katika timu yao.

"Niruhusu nimkaribishe katika timu ya usimamizi mkurugenzi na meneja mpya Frida Kajala. Nimefurahi kufanya kazi na wewe shem," Choppa alitangaza kupitia Instagram.

Kajala aliungana na Chopa, Mjerumani na Jose Wamipango katika timu ya usimamizi wa Harmonize na Konde Gang Music Worldwide.

Haya yalijiri wiki chache tu baada ya Harmonize kusema angependa sana mama huyo wa binti mmoja awe meneja wake.

Baadaye,Harmonize alichapisha ujumbe mrefu akimshukuru muigizaji huyo kwa kusimama naye katika hali zote licha ya mabaya aliyomtendea.

"Wakati Dunia Nzima inasema Haiwezekani Ulisimama Ukasema Inawezekana. Ulinipenda nami mbaya zaidi Ulikutana na Disappointment ambayo iliwapa nguvu na ujasiri kila mtu aliye karibu yako kusema mimi sio binadamu wa kuwa hata karibu yako. Najua uliumia sana ...!!!! Bado hukunikatia tamaa.

"Wakati Mwingine binadamu huingia kwenye mahusiano ukiamini kwamba unaweza kumsahau yule uliyekuwa naye mwanzo bila kuwaza niini kiliwafanya muwe pamoja.

"Nilipitia hicho kipindi na picha zikamwagika mtandaoni na nikajiona nimemaliza wala sikujali maumivu yako. Bado ulikaa kimya, hakuna mahojiano licha ya kuahidiwa marundo ya pesa ambayo ungeweza kununua hata hivyo vigari wanavyoviona ni kitu cha maana sana," Harmonize aliandika chini ya picha ya Kajala ambayo aliipakia hivi karibuni Instagram.

Aidha,ujumbe huo wa Harmonize ulimfikia mlengwa kwani chini yake Kajala alijibu kwa emoji zinazoashiria pongezi na upendo siku hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news