Juma Mgunda ndiye Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa Novemba

NA DIRAMAKINI

KOCHA wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Juma Mgunda amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Novemba, 2022.

Mgunda amewashinda Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Mexime wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba, mwaka huu Kocha Mgunda amewaongoza Simba SC kushinda mechi nne na kutoka sare mbili kati ya sita walizocheza.

Mechi nne walizoshinda ni dhidi ya Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania na walitoka sare dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars.

Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa Mgunda kushinda tuzo ya kocha bora wa mwezi tangu ajiunge na kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi, mwezi Septemba, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news