TANZIA:Mwanahabari mkongwe Shermax Shabaan Ngahemela afariki

NA DIRAMAKINI

MWANDISHI wa habari mkongwe nchini Tanzania, Bw.Shermax Shabaan Ngahemela (pichani) ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Adam Shermax ambaye ni mtoto wa marehemu, baba yake alifikwa na umauti jana jioni Desemba 4, 2022.

Aidha,maziko yatafanyika leo Jumatatu ya Desemba 5, 2022 saa 10 jioni katika Makaburi ya Kisutu yaliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Kwa taarifa zaidi au atakayehitaji kuwasiliana na familia ya marehemu Shermax Shabaan Ngahemela, atumie namba ya simu 0735 764695, ambayo ni ya mtoto wake Adam.

Ramani ya kufika msibani

Ukitokea taa za kuongozea magari za Sayansi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, fuata njia ya kutoka Kijitonyama kutokea kwa Mtogole, pita Shule ya Msingi Kijitonyama, endelea mbele shuka bondeni na unapoanza kupandisha kilima utakuta maegesho ya Bajaji upande wa kushoto, hapo uliza ofisi za Kijiko utakuwa umefika.

Uongozi wa DIRAMAKINI unawapa pole, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao huyo. Mwenyenzi Mungu amlaze mahali pema. Amen.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news