Waziri Prof.Mkenda:Tunathamini sana mchango wenu katika elimu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameishukuru Serikali ya Finland kwa namna ambavyo imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza sekta ya elimu, Sayansi na Teknolojia hususan ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu vikuu na ufadhili wa miradi kupitia taasisi.
Waziri Mkenda ameeleza hayo jijini Dodoma alipokutana na Waziri wa Finland anayeshughulikia masuala ya Uchumi Mhe. Mika Lintila na ujumbe wake.
Amesema, kwa sasa nchi ya Tanzania inafanya mapitio ya Sera ya elimu ya mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala kwa kuhakikisha elimu inatoa ujuzi bila kuathiri ubora katika taaluma.

"Finland mnafanya vizuri sana kwenye elimu ninaomba ushirikiano uliopo uendelee hasa katika kipindi hiki ambacho tunafanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa elimu,"amesema Prof.Mkenda.
Amesema, Serikali pia inaweka utaratibu wa kuwezesha watanzania wengi kwenda kusoma katika vyuo vya nje ikiwemo Sweden ili kupata uzoefu zaidi.
Kwa upande wake Waziri, Mika Lintila amemuhakikishia Waziri Mkenda kuwa ushirikiano wa muda mrefu baina Tanzania na Finland tangu mwaka 1962 utaendelea na kwakuwa uchumi unategemea sana elimu hivyo umuhimu wa kushirikiana katika eneo hili pamoja na teknolojia upo na utaendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news