Biashara Darajani Souk saa 24

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa maduka 452 wa Darajani Souk.
Akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla hiyo Dkt. Mwinyi amepongeza mashirikiano yaliyooneshwa na Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi na Chama cha Mapinduzi katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.
Aidha,amewataka watakaosimamia mradi huo pamoja wafanyabiashara watakaokodishwa milango kuhakikisha wanaitunza na kufanya matengenezo pale panapotokea hitilafu badala ya kuacha kuendelea kuharibika.
Amesema, pia kituo hicho cha biashara kitakuwa na ulinzi na miundo mbinu ya taa na kuwataka wafanyabiashara kufanya biashara zao saa 24.
Naye Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa ametoa shukurani za wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa huo kwa Rais wa Zanzibar kwa kufanikisha mradi huo.
Amesema kuwa Serikali ya Mkoa itaendeleza mashirikiano na sekta mbalimbali, wawekezaji na wakandarasiili kuona miradi iliyokusudiwa kutekelezwa katika Mkoa Mjini Magharibi inafanikiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news