TASAF yabadilisha maisha ya Josephine Bruno kupitia Mradi wa Kokoto

NA MWANDISHI WETU

MKAZI wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara ameipongeza TASAF kwa kuendelea kumsaidia kujinasua katika umaskini na kujimarisha kiuchumi katika utekelezaji wa mpango wake wa kunusuru kaya masikini nchini Tanzania.
Mkazi wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma mkoani Mara, Bi. Josephine Bruno akiponda kokoto ambazo uuza kwa watu mbalimbali wanaofanya ujenzi mradi ambao ameuanzisha baada ya kunufaika na fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini kutoka TASAF ambapo sasa anaweza kuendesha maisha yake vizuri tofauti na hapo awali.

Akizungumza Februari 13 ,2023 Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma,Bi. Josephine Bruno ambaye ni mmoja wa wanufaika wa mpango wa kunusuru Kaya masikini chini ya TASAF ambaye ni miongoni mwa wanufaika waliokuwa wakihudumiwa katika mpango huo kwa muda wa miaka 8 amesema fedha hizo zimemsaidia sana kufanikisha shughuli zake kwa urahisi.
Baadhi ya mawe ambayo wamekuwa wakiponda na kutengeneza kokoto kwa ajili ya kuuza.

Aidha, amesema tangu ameingia TASAF amefanikisha malengo yake ya kuponda kokoto mwenyewe na kujipatia faida kupitia pia watu anaowaajiri kwa ajili ya kuponda kokoto ili kuuza, lakini pia kuwasomesha watoto wake.

“Nilikuwa sina mradi wowote,lakini baada ya kupata fedha za TASAF nilianza kufuga kuku, baadae wakafa, hivyo nikaona watanisumbua nikaanza kufuga bata huku nikiuza baadhi na kuingiza kwenye mradi huu wa mawe ambao ninaajiri mtu halafu ninamlipa,” amesema Josephine Bruno.
Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa Ya Musoma Josephine Bruno akizunguma na Bi.Faraja Luhanjo kutoka TASAF wakati alipotembelea mradi wake wa kokoto mjini Musoma.

Ameishukuru TASAF kwa kumwezesha kujipatia mradi huo wa kuponda mawe kwani kwake umekuwa ni endelevu na mkombozi wa maisha yake ambapo unamsaidia katika maisha na familia yake.

Ameongeza kuwa, moja ya manufaa kutoka TASAF imemsaidia mtoto wake wa kiume kumsomeshwa VETA na kuchaguliwa katika kazi ya kuchomelea ambayo mbali ya kuongeza ujuzi wake, lakini pia inampatia kipato japo kuwa ni kidogo kwa sababu bado hajapata ajira.
Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma Josephine Bruno akionesha nyumba yake haipo pichani ambayo iko karibu na mradi wake huo wa kokoto Manispaa ya Musoma.

Amefafanua kuwa, mtoto wake mwingine amemsomesha kwa kupitia pesa ya TASAF ambapo nilikuwa nikiingiza kwenye mradi,"na faida ambayo nilikuwa naipata ndo nikawa naipeleka chuo ili kumlipia ada mtoto wangu hivyo naishukuru TASAF sana,"amesema Josephine.

Josephine ametumia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutolemaa na pesa ya TASAF ikiwemo kufanyia starehe badala yake waitumie katika maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi ili kuwekeza na kiasi cha faida kinachopatikana wawasomeshe watoto.
Mkazi Wa Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma Josephine Bruno akitoa baadhi ya taarifa zake kwa Bi. Faraja Luhanjo kutoka TASAF wakati alipotembelea mradi wake wa kokoto mjini Musomaanayeandika taarifa hizo ni Afisa Mtendaji wa katika moja ya mitaa ya Kata ya Mwisenge Bw Paul Masige Nyambarya.

Hata hivyo,Josephine licha ya kunufaika na TASAF yeye pamoja na wenzake wanaondoka kwenye mfumo wa huduma hiyo baada ya kuhitimu na uchumi wao Kuimarika Sasa wanaendelea na shughuli zao ndogondogo za kujiongezea kipato na kuendesha maisha Yao

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news