MDAU WA MAENDELEO AMUUNGA MKONO PROF.MUHONGO, ACHANGIA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI SEKONDARI ZA MUSOMA VIJIJINI

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof. Sospeter Muhongo ameshuhudia mmoja wa wadau wa maendeleo hapa nchini, Nguvu Moja Security Service ambaye amechangia shilingi milioni 3.52 kwa ajili ya ujenzi wa MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI (physics, chemistry & biology laboratories) kwenye baadhi ya sekondari za Musoma Vijijini.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. Ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa, mdau huyo wa maendeleo amekabidhi michango hiyo Machi 8, 2023 ikiwa ni hatua muhimu ya kuhakikisha masomo ya sayansi yanasomwa kwa ufanisi ili yachangie katika maendeleo. 

"Mwakilishi wao, Afisa wa Polisi mstaafu, ASP Moyo amekabidhi mchango huo kwenye Duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Musoma Mjini. Mbunge wa Jimbo, Prof. Sospeter Muhongo, alikuwepo kushudia tukio hilo. 
"Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya Sekondari 25 za Kata, 2 za binafsi (madhehebu ya dini).

"Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anahamasisha na kuchangia ujenzi wa Mabaara za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote 27. Lengo kuu ni kuwapatia wanafunzi wa sekondari zetu fursa nzuri ya kupata elimu ya vitendo, na kuongeza uelewa wao wa masomo ya sayansi. Vile vile, ujenzi huu wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ni matayarisho yetu ya kuanzisha high schools za Masomo ya Sayansi jimboni mwetu,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo. 
Sekondari tatu zilizopokea saruji kwa ujenzi wa maabara zao ni Seka Sekondari imepokea saruji mifuko 51, haina maabara hata moja ilifunguliwa mwaka 2021, wanafunzi 344,walimu 7, hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira.

Aidha, Bwai Sekondari imepokea saruji mifuko 51,haina maabara hata moja na ilifunguliwa mwaka 2023 wanafunzi 139, walimu 5, hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Kiriba.

"Muhoji Sekondari imepokea Saruji Mifuko 51, Sekondari mpya inajengwa ifunguliwe mwakani (2024), hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema."
"Tunakukaribisha uchangie ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye shule za Musoma Vijijini."imeeleza taarifa hiyo,"imeongeza taarifa hiyo.

Picha juu zinaonesha sekondari tatu za Musoma Vijijini zikikabidhiwa saruji mifuko 153 kutoka Nguvu Moja Security Service yenye makao makuu jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news