Waislam waanza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan

NA DIRAMAKINI

MUFTI wa Tanzania,Mheshimiwa Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally ametangaza kuanza rasmi kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuanzia Machi 23, 2023.

"Mwezi umeandama leo Jumatano Machi 23, 2023 na hivyo kuashiria kuwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaanza kesho,"amesema Mufti wa Tanzania, Dkt.Abubakar.

Wakati huo huo,Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar nayo pia imetangaza kuandamwa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya Machi 23, 2023 na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imeeleza kuwa, "Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imewataarifu Waislamu wote wa Zanzibar kuwa mwezi umeandama. Hivyo Alhamisi Machi 23, 2023 ni sawa na mwezi 1 wa Ramadhan,"imebainisha taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news