Waziri Dkt.Gwajima aungana na Menejimenti ya wizara kumuaga bosi wa UNICEF Tanzania

NA MWANDISHI WETU
WMJJWM, Dodoma

LEO Mei 29, 2023 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ameiongoza Menejimenti ya wizara hiyo kumuaga aliyekuwa mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF nchini Tanzania, Shalini Bahuguna katika ofisi za wizara jijini Dodoma.
Waziri Dkt. Gwajima amemshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Wizara kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka 2023 alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya watoto nchini.
Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametumia fursa hiyo kumkabidhi Bi. Shalini zawadi mbalimbali ikiwemo cheti cha kuthamini na kutambua mchango wake.
Kwa upande wake, Bi. Shalin licha ya kuishukuru wizara kwa ushirikiano, ameipongeza kwa utendaji, Ubunifu na uendeshaji wa weledi wa kwenye programu za mbalimbali katika kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la UNICEF Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news