Rais Dkt.Samia awapangia Mabalozi vituo vya kazi

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi watatu (03) na amembadilishia kituo cha kazi Balozi mmoja kama ifuatavyo:

Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi:

i) Balozi Khamis Mussa Omar kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China. Bw. Omar anachukua nafasi ya Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

ii) Balozi Ceaser Chacha Waitara kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia. Bw. Waitara anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Modestus Kipilimba ambaye amestaafu.

iii) Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya. Balozi Kibesse anachukua nafasi ya Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.

Balozi aliyehamishiwa kituo:
i) Balozi Mbelwa Brighton Kairuki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uingereza. Balozi Kairuki anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye amemaliza mkataba wake.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 16,2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news