Tanzania, Cuba zakubaliana mambo muhimu

DAR ES SALAAM-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha misingi ya kisiasa, ujengaji wa uwezo kwa wanasiasa vijana, sekta za elimu, afya, utalii, biashara na uwekezaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Cuba nchini, Yordenis Despaigne Vera katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

“Tanzania imekuwa ikishirikiana na Cuba kwa muda mrefu na ushirikiano baina ya mataifa haya umekuwa imara tangu ulipooasisiwa na viongozi wakuu wa Mataifa hayo Hayati Fidel Castro na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,” amesema Balozi Mbarouk. 

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa kwa sasa Cuba imeonesha dhamira ya kushirikiana Tanzania katika kuimarisha misingi ya siasa, kuwajengea uwezo wanasiasa vijana pamoja na sekta nyingine kama vile elimu, afya, na utalii pamoja na kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Cuba.

Kwa upande wake Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera amesema kwamba Cuba inajivunia kuwa na uhusiano imara na Tanzania kwa takribani miaka 60. 

Cuba itaendelea kushirikiana na Tanzania kuimarisha misingi ya kisiasa kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili. “Wakati umefika sasa kwa serikali zetu mbili (Cuba na Tanzania) kuimarisha ushirikiano wake kisiasa na kuhakikisha kuwa mataifa yetu yanakuwa na misingi imara ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi pia kwa manufaa ya pande zote mbili,” amesema Balozi Vera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news