Naibu Waziri Mwanaidi akabidhi mipira ya maji

ZANZIBAR-Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amekabidhi mipira ya maji kwa wakazi wa eneo la Mpapa lililopo Wilaya ya Kati ikiwa ni ahadi yake ya kutatua changamoto za upatikanaji wa maji katika eneo hilo.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, akikabidhi mipira ya maji katika eneo la Mpapa Zanzibar, ambao walikuwa na changamoto ya maji, hii ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wakazi wa eneo hilo.

Naibu Waziri Mwanaidi,Septemba 26, 2023 akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amekabidhi mipira ya maji huku akiwaeleza wananchi kuwa, Serikali ina dhamira ya dhati kuendelea kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo ya maji.

“Niliahidi wakati wa ziara yangu, hii leo naitimiza kwa kukabidhi mipira hii, ili kuhakikisha kunakuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji, niwatakie kila lenye kheri katika kutunza mipira hii na endeleni kuiunga mkono Serikali yetu yenye nia dhabiti katika kuhakikisha uwepo wa huduma muhimu za kijamii,” alisema Mhe. Mwanaidi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na wakazi wa eneo la Mpapa Zanzibar wakati wa zoezi la kukabidhi mipira ya maji iliyotolewa na Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.

Aliongezea kuwa, hii ni sehemu ya kuunga jitihada za Mhe. Rais ya kumtua mama ndoo kichwani na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi kwa kuondokana na changamoto zinazoweza kuwakwamisha katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga aliwakumbusha wakazi hao kuitunza mipira hiyo pamoja na kuwasihi kushirikiana kwa umoja katika masuala mbalimbali ya maendeleo nchini.
Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Kati Mhe. Khadija Kassim akitoa shukrani kwa Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis mara baada ya kukabidhiwa mipira ya maji katika eneo la Mpapa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wakazi hao, amekabidhi tarehe 26 Septemba, 2023.

Naye Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Kati, Mhe. Khadija Kassim akitoa shukrani kwa Naibu Waziri huyo alisema wamefarijika na kuendelea kuipongeza Serikali kwa kutatua changamoto zinazowakabili huku akitoa neno kwa wakazi hao kuunga mkono juhudi za Serikali yao.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis Pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga wakiwa katika picha ya Pamoja na wakazi wa eneo la Mpapa Zanzibar mara baada ya kukabidhi mipira ya maji kwa wananchi hao.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

“Binafsi naendelea kumpongeza sana Naibu Waziri Mwanaidi kuona umuhimu na kutuvusha katika hili, hii imekuwa historia kwetu, tunaona jitihada hizi kwa matendo siyo kwa huduma za maji tu, hata masuala ya afya, nishati na nyingine nyingi,”alisema Mhe. Khadija.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news