Waziri Mkuu ashiriki uapisho wa Rais Mnangagwa

HARARE-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 04, 2023 ameshiriki sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika uwanja wa Harare, Zimbabwe.

Mheshimiwa Rais Mteule Mnangagwa ameshinda uchaguzi huo kwa kura zaidi ya milioni 2.3 kati ya kura milioni 4.4 zilizopigwa sawa na asilimia 52.6 dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa ambaye alipata kura milioni 1.9 sawa na asilimia 44.

Ushindi huo unamfanya Mheshimiwa Mnangagwa kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.

Mheshimiwa Majaliwa amemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho huo.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news