Kamati kuchambua miswada miwili ya sheria

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepanga kuchambua Miswada miwili ya Sheria iliyopelekwa kwenye Kamati hiyo.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellanaous Amendments) (No.4)Bill, 2023] na Muswada ya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Sekta ya Sheria wa Mwaka 2023 [The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023].

Katika kutekeleza jukumu hilo na kwa mujibu wa Kanuni ya 97 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023, Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Alhamisi tarehe 19 Oktoba, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Frank Mfundo, Ghorofa ya 5 Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imepanga kufanya Mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu Azimio la Bunge la Mapendekezo ya Tanzania Kuridhia Kujiunga na Mkataba wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu wa Mwaka 2009 (Statute of The International Renewable Energy Agency – Irena).

Kamati inatekeleza jukumu hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 108 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023 Kamati itasikiliza na kupokea maoni ya wadau (Public Hearing) siku ya Alhamisi tarehe 19 Oktoba, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Msekwa kwenye Jengo la Pius Msekwa, Jijini Dodoma.

Kamati zinawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Miswada na Azimio hilo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla kupelekwa katika hatua nyingine.

Vilevile Kamati zitapokea maoni kwa njia ya Posta au Barua Pepe kwa anuani ifuatayo: -
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
10 Barabara ya Morogoro,
S.L.P. 941,
41105 Tambukareli,
DODOMA.
Baruapepe:
cna@bunge.go.tz na
kamati@bunge.go.tz

Miswada na Azimio hilo vinaweza kupakuliwa katika Tovuti ya Bunge,www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news