MSD yakabidhi dawa, vifaa tiba vya milioni 349.2/- Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara

MANYARA-Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 349, 167 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma hospitalini hapo.
Akiongea wakati wa kupokea bidhaa hizo, Mfamasia wa hospitali hiyo, Bi.Shukuru Robert ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma hospitalini hapo.
Aidha, ameipongeza Wizara ya Afya chini ya Mhe. Ummy Mwalimu kwa uongozi na usimamizi thabiti wa sekta ya afya.
Bi. Shukuru amebainisha kwamba wamepokea, vitanda vya umeme, magodoro, mashuka, viti vya magurudumu pamoja na dawa za aina mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news