EWURA yatangaza bei kikomo za mafuta Novemba 2023, hizi hapa bei zote nchini

DAR ES SALAAM-Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 1 Novemba 2023 saa 6:01 usiku.

Dkt. James A. Mwainyekule ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA amefafanua kuwa, kwa mwezi Novemba 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam lita ya Petroli inauzwa kwa shilingi 3,274 huku Dizeli ikiuzwa kwa shilingi 3,374 na Mafuta ya Taa lita shilingi 3,423.

Kwa Mkoa wa Tanga lita ya Petroli inauzwa kwa shilingi 3,320 huku Dizeli ikiuzwa kwa shilingi 3,510 na Mafuta ya Taa lita inauzwa kwa shilingi 3,469.

Mkoa wa Mtwara mafuta ya Petroli yanauzwa shilingi 3,347 kwa lita huku Dizeli ikiuzwa kwa shilingi 3,546 na Mafuta ya Taa yanauzwa kwa shilingi 3,495.

Dkt.Mwainyekule amefafanua kuwa, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Novemba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 5.68 na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 13 kwa petroli.

Sambamba na asilimia 25 kwa dizeli na uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa.

Bei za mafuta katika miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1 na bei za mafuta kwa wafanyabiashara wa jumla ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.

Dkt.Mwainyekule amesema, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 1.

Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka agizo hili. EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: -

a) bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023.

d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.

Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa.

Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.

JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA KWA SHILINGI/LITA







Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news