Waziri Makamba apokea nakala za hati za utambulisho za Balozi mteule wa Libya nchini

DAR ES SALAAM-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Libya nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul Alshatewi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akipokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Libya nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul Alshatewi katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Makamba amemkaribisha nchini Mhe. Alshatewi na kumuahidi ushirikiano wa Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote atakaokuwa akitekeleza majukumu yake nchini.

Aidha, Waziri Makamba ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Libya umedumu kwa zaidi ya miaka 50 na na wakati wote umekuwa imara. “Tunaamini kuwa Mhe. Balozi wakati wa uwakilishi wako uhusiano baina ya mataifa yetu utaendelea kuimarika zaidi katika sekta mbalimbali za kimkakati,” aliongeza Waziri Makamba.

Kwa upnade wake Balozi Mteule, wa Libya nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul Alshatewi amesema kuwa atafanya kazi kwa ushirikiano na Tanzania wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Libya nchini, Mhe. Abulmajed Albhloul Alshatewi pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maafisa kutoka Ubalozi wa Libya baada ya Balozi Mteule kuwasilisha nakala za hati za utambulisho.

"Ni faraja kwangu kuja kufanya kazi Tanzania naahidi wakati wote wa uwakilishi wangu hapa Tanzania kama Balozi tutafanya kazi kwa ushirikiano katika kunendeleza sekta mbalimbali hususan biashara na uwekezaji, kilimo na nyingine."

Katika tukio jingine, Waziri Makamba amekutana kwa Mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Didier Chassot, Balozi wa Vatican nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini, Bw. Robert Raines.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Makamba amejadiliana na Mabalozi hao masuala mbalimbali ya ushirikiano wa uwili, kikanda na ushirikiano wa kimataifa baina ya Tanzania na nchi zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news