Baada ya kuwekewa puto Mloganzila nimepungua kutoka kilo 150 hadi 99-Vicent Fortunatus

DAR ES SALAAM-Bw. Vicent Fortunatus amesema huduma aliyowekewa ya puto maalumu (intragastric balloon) pamoja na kupunguza zaidi ya kilo 50 imekuwa na mafanikio makubwa.

Vile vile kuondokana na changamoto ya maumivu ya mgongo, mwili kuwa mwepesi na kuwa rahisi kwake kutekeleza majukumu ambayo awali ilikuwa ngumu kuyatekeleza.
Bw. Fortunatus ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Prof. Mohamed Janabi katika kipindi cha AFYA PODCAST ambapo amebainisha kuwa, hakuchanwa popote ili kuwekewa puto na ulaji wake umebadilika sana.
Aidha, Prof. Janabi ameihakikishia jamii kuwa huduma hiyo ni salama na inatumia teknolojia ya hali ya juu duniani ambapo dhumuni lake ni kumtengenezea mtu utamaduni wa kula kidogo.

Pia,kuzingatia mlo kamili kwa kuwa puto linakuwa limechukua moja ya tatu ya tumbo na mbili ya tatu inabaki kwa ajili ya chakula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news