Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (USAFRICOM) yaipa saluti DCEA kwa udhibiti dawa za kulevya Tanzania

DAR ES SALAAM-Naibu Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (USAFRICOM),Balozi Robert Scott ametembelea ofisi za Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa lengo la kuipongeza mamlaka na kutambua kazi kubwa inayofanyika baada ya ukamataji wa zaidi ya tani tatu za dawa za kulevya uliofanyika nchini hivi karibuni.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》
Ziara hiyo imefanyika Julai 26,2024 katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Aidha, kwa niaba ya Mkuu wa Kamandi hiyo Jenerali Michael Langley, Balozi Scott amemkabidhi Kamishna Jenerali Aretas Lyimo cheti kwa kutambua juhudi hizo.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》

Ziara hiyo inakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) ikamate jumla ya tani 3.182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphemine zikiwa kwenye vifungashio vya kahawa na majani ya chai.

Dawa hizo zilikamatwa katika operesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya Desemba 5 hadi 23, 2023.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》

Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali, Aretas Lyimo alisema, tangu udhibiti uanze DCEA haijawahi kukamata kiasi kikubwa cha dawa kama ilivyo sasa na iwapo zingefanikiwa kuingia sokoni watu milioni 76.3 wangeathirika.
“Ukamataji huu umeokoa nguvu kazi yaani Tanzania tupo idadi ya watu milioni 60 hizi dawa zingefanikiwa kuingia sokoni basi zingeathiri si tu Watanzania bali hata mataifa mengine maana nyingine zilikuwa zikisafirishwa nchi nyingine,”alisema Kamishna Jenerali Lyimo.

Alibainisha kuwa, kiasi hicho cha dawa kinajumuisha kilogramu 2, 180.29 za dawa aina ya Methamphemine na kilogramu 1001.71 aina ya Heroin zilizokamatwa katika wilaya za Kigamboni, Ubungo na Kinondoni kwa jijini Dar es Salaam na mkoani Iringa.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》

Kamishna Jenerali Lyimo alisema, katika operesheni hiyo watu saba walikamatwa kati yao wawili ni raia kutoka bara la Asia.

Aidha, Kamishna Jenerali Lyimo alisema, mbinu ambayo imekuwa ikitumika kufunga dawa hizo kwenye vifungashio vya bidhaa zenye chapa mbalimbali ikiwemo kahawa na majani ya chai inatumika kwa lengo la kurahisha usafirishaji wake na kukwepa kubainika.
Alisema, dawa ya Methamphemine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa na cocaine.

“Dawa hii huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembechembe mithili ya chumvi ang’avu yenye rangi mbali lmbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubu kwa kuchanganya aina mbali mbali za kemikali bashirifu,”alisema Kamishna Jenerali Lyimo.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》

Alisema, mamlaka inatoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini kuacha badala yake wajikite kwenye biashara nyingine halali kwani DCEA imejidhatiti kukomesha biashara ya dawa ya kulevya nchini.
“Mamlaka inaishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha mamlaka katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi mkubwa,”alisema Kamishna Jenerali Lyimo.DCEA yamdaka kinara wa dawa za kulevya》》》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news