DODOMA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kati imeshiriki katika mafunzo ya usimamizi salama wa kemikali kwa wadau wa kemikali wa kanda hiyo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati.
Katika mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi wa Sayansi Jinai wa DCEA, Ziliwa Machibya, amewasilisha mada kuhusu kemikali bashirifu na madhara ya uchepushaji wa kemikali hizo.
Akizungumzia mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Kanda, Dkt. Christian Mbwasi, amesema, mamlaka itaendelea kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na wadau wa kemikali katika kuhakikisha wanasimamia kwa usahihi na kuzuia uchepushwaji.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)