Rais Dkt.Samia aomboleza vifo 21 mgodini

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa masikitiko taarifa ya vifo zaidi ya 21 mgodini.
Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ameyabainisha hayo leo Januari 14,2024 kupitia taarifa aliyoitoa katika kurasa zake rasmi za kijamii.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 21 kufuatia ajali ya kufunikwa na ardhi katika Mgodi wa Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

"Ndugu zetu hawa walikuwa wachimbaji wadogo katika eneo hili, wakijitafutia riziki zao, familia zao na kuchangia maendeleo ya taifa letu.

"Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao katika ajali hii.

"Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi,"amefafanua Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news