Endeleeni kulinda amani na mshikamano wa Taifa letu-Waziri Mhagama

NJOMBE-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuzilinda tunu za umoja wa kitaifa za utulivu, amani na ushirikiano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama akimpongeza Mhashamu Askofu Dkt. Eusebius Kyando Askofu wa Jimbo la Njombe, mara baada ya ibada ya kuwekwa wakfu leo Januari 14,2024.
Rai hiyo ametoa wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Misa ya kuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Njombe Dkt. Eusebius Samwel Kyando iliyofanyika Mkoani Njombe tarehe 14 Januari, 2024.

Waziri amesema kuwa tunu hizo ndizo zinazotambulisha Taifa letu la Tanzania duniani na ulimwenguni kote.

"Tunu hizi zilindwe kwa kuzingatia umuhimu wake, pia Serikali inashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa, tunaomba muendelee kuliombea bila kuchoka," alifafanua Waziri.
Aidha, viongozi wa dini mmekua mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa katika hali ya utulivu mstahimilivu na Mhe. Rais amekuwa mstari wa mbele Kati Jambo hilo.

"Niwaombe sana viongozi wa dini tuendelee kukemea pale tunapoona kuna viashiria vya watu wachache kuvunja amani, utulivu umoja na mshikamano wa Nchi yetu," alihimiza.
Aidha,aliitaka jamii kuungana na Serikali katika kupaza sauti juu ya matendo maovu na hasa mauaji na ukatili wa kijinsia, imani potovu ambazo zinapelekea mauaji na unyanyasaji wa watoto wadogo.

Akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka ameomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika sekta ya elimu hasa katika masuala ya lishe kwa wanafunzi mashuleni katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo.

"Hii itasaidia kuleta hamasa kuwaandaa watoto kwa kuwapatia lishe Bora ambayo itawasaidia kufanya vizuri katika maisha yao,"amesema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka wakiwa katika picha ya pamoja na Mhashamu Askofu Dkt. Eusebius Kyando mara baada ya ibada ya kumweka wakfu askofu huyo.

Kwa upande wake mmoja wa waumini wa kanisa hilo Bi, Naomi Nzota amesema waumini wa Jimbo la Njombe wamefurahi Sana kwa kupata, Askofu Dkt. Eusebius Kyando baada ya Misa wa kuweka wakfu iliyoongozwa na Muasham AsAskofmstaafu wa Jimbo la Dar eseDalaam, Polcapy Pengo.

"Ameueleza utumishi wa Askofu Dkt. Eusebius Kyando kwamba ni mtumishi, mnyenyekevu mnyoofu na mvumilivu,"alieleza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news