Serikali yajenga madarasa Lupilinga

RUVUMA-Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Lupilinga iliyopo Kata ya Lukarasi ni moja ya mfano wa utekelezaji huo ambao umetekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na nguvu za wananchi.

Halmashauri imetoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya kuendeleza maboma ya madarasa ambayo yalijengwa kupitia nguvu za wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news