Wizara yatoa wito kwa Wakufunzi

ZANZIBAR-Wakufunzi wa Mafunzo ya Ualimu wametakiwa kuwaandaa walimu wa Skuli za Maandalizi na Msingi ili waweze kutumia mbinu bora katika kufundisha.
Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Mwalimu Moh’d Nassor Salim wakati akifungua warsha ya siku sita iliyowashirikisha Wakufunzi wanaotarajiwa kuwafundisha Walimu wa Skuli za Maandalizi na Msingi huko katika Ukumbi wa Kituo cha Walimu Michakaeni Chake chake Pemba.

Amesema, kupitia warsha hiyo Wakufunzi hao wataweza kujadili mbinu mbalimbali zitakazowazaidia walimu kuwaandaa Wanafunzi kiumahiri.
Aidha, amewahakikishia Wakufunzi hao kwamba kupitia Mageuzi ya Elimu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu inaandaa mkakati wa kuanzisha Chuo cha Ualimu kinachojitegemea.

Mwalimu Moh’d amefafanua kuwa,uwepo wa chuo hicho itakuwa chachu ya kuzalisha walimu waliobobea katika fani ya Ualimu na ambao watafanya kazi kwa uzalendo Zaidi.
Naye Katibu wa Baraza la Elimu na Mrajisi wa Elimu Zanzibar, Hafsa Abood Talib ameelezea matumaini yake kwa Wakufunzi hao kuyashusha vyema mafunzo hayo kwa Walimu ili Wanafunzi waweze kupata taaluma mbali mbali.

Amesema, kwa kuwa mtaala mpya unalenga kuwaandaa wanafunzi kiumahiri hivyo mafunzo hayo ya siku sita yatawajengea uwezo Wakufunzi hao kwenda kuwaandaa Wanafunzi kufikia malengo ya Mtaala huo.
Akiwasilisha mada Kuhusu taaluma za Karne ya 21 Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,Bi. Mariam Amour Mwinyi amewataka wakufunzi hao kuwaandaa walimu kuweza kufundisha taaluma mbalimbali ili wanafunzi waweze kuzitumia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news