Dkt.Shelukindo aongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki ISPDC ya SADC

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kamati ya Siasa na Diplomasia (Inter-State Politics and Diplomacy Committee-ISPDC) ya SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao leo Februari 9, 2024.
Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Zambia, Bi. Etambuyu Gundersen ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.

Mkutano huo uliitishwa kujadili masuala ya kisiasa na diplomasia katika kanda.
Aidha, mkutano umetoa salamu za pole kwa Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Namibia kufuatia kifo cha Hayati Dkt. Hage Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kilichotokea hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news