Mashabiki waiponza Simba SC

DAR ES SALAAM-Bodi ya Ligi (TPLB) imeipiga faini ya shilingi milioni mbili Simba SC katika matukio mawili tofauti yanayohusu michezo yake ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 15, 2024 na Shirikisho la Mpira wa Miguu ( TFF).

Simba imepigwa faini ya kwanza ya shilingi milioni moja kwa kosa la mashabiki wake kumwaga vitu vyenye asili ya unga katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Ni kabla ya wachezaji hawajaanza kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Tabora United.

Tukio hilo limetafsiriwa kama vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

Imeeleza kuwa, pia Simba imetozwa faini nyingine ya shilingi milioni 1 kwa kosa la mashabiki wake kuingia katika eneo la kuchezea baada ya mchezo dhidi ya Azam FC uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

TFF imeeleza kuwa, adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni ya 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news