Rais Dkt.Mwinyi:Tumuenzi Lowassa kwa uzalendo na uwajibikaji

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema, namna bora ya kumuenzi Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Februari 13, 2024 jijini Dar es Salaam alipotoa salamu za pole na kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Vile vile, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ametoa salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na wananchi wote kwa msiba huo.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, amejifunza mengi kutoka kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele maslahi ya nchi. Tafadhaili, msikilize Rais Dkt.Mwinyi kupitia video hapa chini;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news