Msajili wa Hazina ajumuika na Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa Lowassa

DAR ES SALAAM-Leo Februari 13, 2024 Msajili wa Hazina, Nehemiah Kyando Mchechu amejumuika na viongozi pamoja na wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa.
Msajili wa Hazina, Nehemiah Kyando Mchechu akisaini kitabu cha maombolezo leo Februari 13, 2024 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo amejuimuika pamoja na viongozi na wananchi katika kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa. 

Tukio hilo limeongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ambapo ametoa salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa familia, ndugu, marafiki pamoja na watanzania wote kwa ujumla kufuatia msiba huo mkubwa kwa Taifa.

Edward Ngoyai Lowassa alifariki Februari 10, 2024 wakati akiendelea na matibabu jijini Dar es Salaam huku akitarajiwa kuzikwa kijijini kwao huko Monduli jijini Arusha siku ya Februari 17, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news