Rais Dkt.Samia abainisha namna ya kumuenzi Lowassa

ARUSHA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema, miongoni mwa vitu alivyojifunza kutoka kwa hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kiongozi ambaye ukimheshimu anakuheshimu pia.

“Nilijifunza mengi kutoka kwake (hayati Edward Ngoyai Lowassa). Kati ya hayo, nililoliona kwa mheshimiwa Lowassa ni kwamba ukimheshimu, anakuheshimu.”

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Februari 17, 2024 wakati akitoa neno la pole kwa familia ya aliyekuwa Lowassa wakati wa maziko yake kijijini kwake Ngaresh wilayani Monduli mkoani Arusha.

Pamoja nna hilo,Rais Samia amesema Lowassa hakuwahi kuwasema vibaya wapinzani wake wa kisiasa pindi alipoamua kuhama chama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news