Rais Dkt.Samia awaongoza Watanzania maziko ya Lowassa

AUSHA-Rais wa Jamhuri waMuunagano wa Tanznia,Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza maelfu ya waombolezaji katika maziko ya hayati Edward Ngoyai Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ngalash Wilayani Monduli.

Akitoa salamu za rambirambi, Mhe. Rais, amewataka Watanzania kuendelea kumkumbuka hayati Lowassa kwa mengi mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake, ikiwemo Siasa za kistaarabu kwa maslahi mapana ya Taifa.

Rais Samia aliongeza kusema kuwa, katika sekta ya elimu hayati Edward Lowassa alisimamia kwa weledi mkubwa mpango waMaendeleo yaElimu ya Secondari akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, katika Serikali ya awamu ya nne katika kuratibu na kusimamia kwa umakini ujenzi wa shule za sekondari katika Kata zote nchi nzima.

Aidha Mhe. Rais Samia alifafanua kuwa, tangu wakati huo serikali imeendelea kusimamia ujenzi wa shule hizo na usimamizi wa kuziendeleza kata zote nchini na kufanya ongezeko la shule za Serikali kutoka 828 mwaka 2004 hadi kufikia 4578 mwaka 2023.

Akihitimisha salam za rambirambi, Rais Samia amesema Taifa litaendelea kumkumbuka Haayati Lowassa kwani limepoteza kiongozi mahiri na shupavu, mwanamageuzi, mpenda maendeleo na aliyekuwa kipenzi cha watu.

Viongozi wa Kitaifa wengine waliyoshiriki Maziko ya Hayati Lowassa ni Mhe. Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais, Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mazishi ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news