Sagini atoa maelekezo ajali iliyoua 25 Arusha

NA ABEL PAUL
Tanpol

NAIBU-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimimiwa Jumanne Sagini amefika jijini Arusha na kukagua eneo la ajali iyotokea Februali 24, 2024 katika barabara ya Arusha - Namanga, Eneo la Ngaramtoni kibaoni wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mheshimimiwa Jumanne Sagini pamoja na kutoa pole kwa waathirika wa ajali hiyo, amelitaka Jeshi la Polisi kuweka mikakati madhubuti ya ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya nchi pamoja na yale yaliyopo ndani ya nchi pasipo kusubiria wiki ya nenda kwa usalama ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uzembe wa madereva ama ubovu wa magari.
Aidha,Mheshimiwa Sagini ametoa pongezi kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Wa Arusha Mount Meru, madaktari, wauguzi pamoja na Jeshi la Polisi na kwa namna walivyotoa huduma bora kwa majeruhi waliopata ajali siku ya jana.

Amefafanua kuwa, ajali hiyo imehusisha raia wa kigeni kutoka nchi za Marekani, Afrika Kusini, Nigeria, Togo, Bukinafaso, Madagasca na Kenya.
Pia ametoa salamu za pole toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.  Samia Suluhu Hassan kwa watanzania hususani wananchi wa Mkoa wa Arusha kufuatia ajali hiyo.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP. Awadh Juma Haji amesema amepokea maelekezo yalitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuwa watayafanyia kazi ili kuhakikisha watumiaji wa barabara wanafuata sheria za usalama barabarani ikiwemo watembea wa Miguu ili kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa.
CP Awadhi amesema kuwa,katika kuhakikisha wanatokomeza ajali tayari jeshi hilo limeingia makubalino na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kutumia vifaa vya kisasa katika ukaguzi wa vyombo vya moto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news