Wizara ya Maendeleo ya Jamii Zanzibar yaelezea ushiriki wake Mkutano wa MMMAM nchini

ZANZIBAR-Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inarajiwa kuwa mdau katika Mkutano wa Kimataifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) unayotarajiwa kufanyika mwezi Machi, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Akizungumza ofisini kwake Kinazini Unguja na viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Bi. Abeida Rashid Abdallah amesema,wizara hiyo imefanya jambo jema kuishirikisha wizara yake kuwa mdau katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 11-14 Machi 2024 katika Ukumbi wa Kimataifa ya Mwalimu Julius Nyerere.

Amesema, ni wazi kwamba Serikali zote mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Jamhuri ya Mungano wa Tanzania (SMT) kwa pamoja zinalengo la kuisaidia jamii katika malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto. Kwani mtoto ndio tegemeo la taifa la kesho.

Aidha bi Abeida ameshauri katika mkutano huo ni vyema kuwashirikisha na Wizara zingine za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ikiwemo Wizara Afya, Elimu na Mafunzo ya Amali kwani Wizara hizo pia ni wadau katika masula ya mtoto.
Pia, Katibu Mkuu Abeida amemshukuru Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Mhe. Dkt. Doroth Gwajima na Katibu Mkuu wake, Dkt.Seif Shekalaghe kwa namna wanavyoshirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (SMZ) katika mambo mengi ya kiutendaji.

“Kupitia mashirikiano hayo wizara yetu inapata mambo mengi ya kuiga, kwani wizara yetu imezaliwa upya, yapo mengine hatuwezi kuiga kwa sababu hayatekeleziki kutokana na nature ya mazingira yetu huwa tunaachana nayo, ila tunawashukuru sana kwa mashirikiano yao kwetu,”amesema Abeida.

Abeida amewataka maafisa watendaji wa pande zote mbili kuendeleza vikao vya mashirikiano kwani vikao hivyo ni muhimu na vinazaa matunda ya maendeleo kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mathias Mgimbe Haule amesema,kupitia mkutano huo uaotarajiwa kufanyika Machi kutawasilishwa mada mbalimbali zinazohusiana na Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto kwani wadau wameshaanza kutuma stakabadhi za kuwasilisha.

Pia amesema, wizara yake inatarajia kuanzisha Madawati ya Watoto ambapo yamelenga kutoa elimu kwa watoto ili waweze kujilinda pamoja na kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kinjisia na udhalilishaji.

Mapemba Mshauri elekezi wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ,Godwin Emil Mongi ameeleza kwamba,Mkutano wa Kimataifa wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) unayotarajiwa kufanyiaka mwezi Machi mwaka huu ni mkutano wa kwanza kwa Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Abeida ya Rashid Abdallah, Mkurugenzi Idara ya Mtoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mathias Haule (kulia) na mashauri elekezi wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto,Godwin Emil kutoka wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika ofisi ya Katibu Mkuu huyo, Kinazini Unguja.

Aidha, alifahamishwa kwamba hadi sasa maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na utarajiwa kuwa washiriki zaidi ya 1500 kwani hadi sasa wadau waliyojisajili wameshafikia idadi ya 1200.

Hivyo ametoa wito kwa wadau wengi kujisajili kabla ya muda wa usajili kumalizika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news