Dkt.Mpango amuagiza Waziri wa Fedha kupitia kodi ya majiko

JOSEPHINE MAJURA NA ASIA SINGANO

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kuangalia uwezekano wa kupitia viwango vya kodi kwa majiko yanayotumia nishati safi ya kupikia hasa kipindi hiki ambacho maandalizi ya bajeti ijayo yanafanyika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika katika Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Tarehe 09 Machi 2024.

Maagizo hayo ameyatoa wakati akifungua Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia, lililofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, aliyekuwa Mgeni Rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya kupikia, lililofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi Wanawake wa Wizara ya Fedha wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha Bi. Fauzia Nombo (wa pili) wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe) Dkt. Philip Isdor Mpango ambae alikuwa Mgeni Rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.

Aidha Mhe. Mpango amezitaka Sekta Binafsi nchini kutumia fursa ya kutokomeza matumizi ya nishati chafu kama njia moja wapo ya kuongeza kipato chao na kukuza uchumi wa nchi.

‘’Natoa wito kwa sekta binafsi kuunga mkono na kuchangia katika kampeni ya kuondokana na matumizi ya nishati chafu. Baadhi ya maeneo ambayo sekta binafsi inaweza kusaidia ni kuwekeza katika utafiti, ubunifu na uzalishaji wa nishati safi na nafuu ya kupikia,’’ alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Aliongeza kuwa matumizi ya nishati chafu kama vile mkaa na kuni yameleta athari kubwa zaidi kiafya kwa wananchi hususani wanawake ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bi. Fauzia Nombo (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wanawake wa Wizara hiyo walioshiriki hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya kupikia iliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma.

‘’Wanawake huvuta moshi mwingi wenye viwango vikubwa vya sumu, ambazo husababisha magonjwa ya mfumo wa hewa yanayosababisha vifo takriban 33,000 vya watanzania kila mwaka’’ alisisitiza Mhe. Dkt. Mpango.

Kongamano hilo limefanyika kama sehemu yakuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha wanawake kutumia nishati safi ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news