Jela miaka 25 kwa kukutwa na kilo 107.29 za bangi

MOROGORO-Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro imemhukumu miaka 25 jela, John Mwaseba Mwasikili baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye ujazo wa kilo 107.29.
Akitoa hukumu hiyo Jaji wa mahakama hiyo, M. P.Otaru amesema, ushahidi uliotolewa na mashahidi 16 na vielelezo 15 vya upande wa mashitaka haukuacha shaka dhidi ya mshitakiwa kutenda kosa hilo.

Jaji Otaru amesema kuwa amemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kujiridhisha kuwa ni kweli mshitakiwa alikamatwa na dawa ya kulevya aina ya bangi yenye uzito wa kilo 107.29 iliyokuwa ndani ya gari aina ya Toyota Kluger namba T.895 CQR kwenye mifuko nane ya sulphate.

Mahakama pia imeamuru gari namba T 895 CQR ambalo lilikuwa na bangi hiyo litaifishwe na kielelezo ambacho ni dawa za kulevya aina ya bangi kuteketezwa.

Mshitakiwa Mwasikili alikamatwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya na kufikisha katika Mahakama kuu kanda ya Morogoro Machi 15, 2024.

Inadaiwa kuwa mwaka 2022 huko Morogoro lilikamatwa gari aina ya Toyota Kluger lenye namba za usajili T.985 ambalo ndani yake lilikutwa na mifuko nane ya sulphate ikiwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news