Dhana potofu kuhusu mbolea yaathiri uzalishaji wa mazao Kanda ya Kati

SINGIDA-Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo amesema,wakulima wa Kanda ya Kati wanazalisha chini ya kiwango kutokana na dhana potofu ya wakulima kuwa Mbolea inaharibu udongo wa mashamba yao.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA Dkt. Anthony Diallo akizungumza na Viongozi na wadau wa kilimo wa mkoa wa Singida wakati wa kikao baina ya Bodi na menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Singida tarehe 17 Aprili, 2024.

Dkt. Diallo amesema hayo wakati akizungumza na Wadau wa Kilimo wa Mkoa wa Singida, ikiwa ni ziara ya Wajumbe wa Bodi na Menejimenti TFRA iliyolenga kutoa Elimu na Kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima.
Amesema, wakulima wengi hawataki kutumia Mbolea kwa kudhani kuwa mbolea inaharibu udongo wa mashamba yao na kuamini kuwa itasababisha wavune mazao kidogo jambo ambalo si kweli.

Dkt. Diallo amesema ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija na mazao mengi katika eneo dogo ni lazima wahimizwe kutumia Mbolea kwa wakati na kwa usahihi, na kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalam wa Kilimo.Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA Dkt. Anthony Diallo akizungumza na Viongozi na wadau wa kilimo wa mkoa wa Singida wakati wa kikao baina ya Bodi na menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Singida tarehe 17 Aprili, 2024.

Pamoja na hayo, Dkt. Diallo amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kufuatilia taarifa ya afya ya udogoya maeneo wanayoyasimamia ili wakulima watumie mbolea kulingana na mahitaji ya udongo wanaoulima. Viongozi na wadau wa kilimo wa mkoani Singida wakifuatilia mada wakati wa kikao baina yao na Wajumbe wa Bodi na menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Singida tarehe 17 Aprili, 2024.

Amesema, taarifa hiyo pia itasaidia wazalishaji kujua aina ya virutubisho vinavyohitajika katika kila eneo la nchi na kuzalisha na kusambaza kiasi cha mbolea kinachotosheleza mahitaji husika.

"Huwezi kutumia Mbolea bila kujua afya ya udongo, hivyo wakulima watumie mbolea kutokana na afya ya udongo wa mashamba yao,"Dkt. Diallo ameongeza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akizungumza wakati wa kikao kilichowakutanisha wajumbe wa Bodi, menejimenti ya TFRA, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wafanyabiashara na wakulima wa Mkoa wa Singida kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya mbolea mkoani humo tarehe 17 Aprili, 2024. Kulia aliyekaa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent amesema Mikoa ya Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa imeendelea kuwa na matumizi madogo ya Mbolea kutokana na mwamko mdogo wa wakulima kutumia Mbolea hali inayosababisha wakulima kuzalisha chini ya kiwango.

Ili kuongeza matumizi ya Mbolea Mkurugenzi Laurent amewataka Maafisa Ugani kuendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu faida za matumizi ya mbolea ili waweze kutumia mbolea na waweze kuongeza uzalishaji.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Allan Mariki akitoa neno la utangulizi katika kikao cha Bodi, Menejimenti ya TFRA na wadau wa tasnia ya mbolea wa Mkoa wa Singida waliohusisha viongozi wa serikali, wafanyabiashara wa mbolea na wakulima kwa lengo la kutoa elimu na hamasa ya kutumia mbolea kwenye shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji mkoani humo.

Aidha, ameahidi Mamlaka kusimamia zoezi la kufikisha Mbolea kwa wakulima kwa wakati ili kuondoa vikwazo vinavyowafanya wakulima kushindwa kutumia Mbolea kwenye uzalishaji wao.

Kwa upande wa baadhi ya wadau wa kilimo walioshiri katika kikao hicho wameomba mbolea hizo ziwe zinawafikia kwa wakati ili kuwaepushia kadhia wanayoipata pindi msimu wa kilimo unapofika na pembejeo hiyo kukosekana sokoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news