Tanzania imepiga hatua kiuchumi na kidemokrasia-Waziri wa Fedha

NA BENNY MWAIPAJA
Washington D.C

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amelihakikishia Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (Millennium Challenge Corporation-MCC) kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora, demokrasia na usimamizi imara wa uchumi wa nchi.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), ukiwa katika mkutano na Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo walijadiliana masuala ya ushirikiano Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga katika mageuzi ya kisera na kitaasisi aili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C.).

Dkt. Nchemba amesema hayo alipoongoza ujumbe wa Tanzania, kukutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Shirika hilo, ukiongozwa na Makamu wake wa Rais Mhe. Alicia Mandaville, Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pande hizo mbili zilijadili namna ya kuharakisha utekelezaji wa mpango wa kusaidia mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kutatua vikwazo vya ukuaji uchumi, kupitia ruzuku itakayotolewa na Shirika hilo.
Uongozi wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ukifuatilia kwa umakini majadiliano kati yake na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), katika Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C, ambapo walijadiliana masuala ya ushirikiano na Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kuleta mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Alisema kuwa hatua hiyo si tu kwamba ni utekelezaji wa vigezo vilivyowekwa na Shirika hilo ili Tanzania iweze kunufaika na mpango huo unaolenga kutoa misaada ya kiufundi, bali ni nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kulinda uhuru wa watu.

Dkt. Nchemba aliihakikishia MCC kwamba Tanzania iko tayari kushirikiana na Serikali ya Marekani katika mpango huo na kuuomba uongozi huo kuuamini mchakato huo na ikiwezekana kuipatia nchi mradi mkubwa wa COMPACT II, utakao iwezesha nchi kupata fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati katika sekta za usafirishaji, nishati, na maji..
Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden (kushoto), akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Uongozi wa Shirika hilo na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani), ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi. Mkutano huo umefanyika kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi, Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, aliahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuanzisha ushirikiano huo wa kimaendeleo kwa kuwa Serikali imepiga hatua kubwa kutimiza vigezo vilivyowekwa ili nchi iweze kunufaika na mpango huo.

Bi. Blyeden alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo ambao matokeo yake hapo baadae utaiwezesha Marekani kurejesha mradi wa Changamoto za Milenia (MCC-Compact) utakao kuwa na lengo la kusaidia nchi kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (hayupo pichani) na Uongozi Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kihusu ushirikiano wa Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kuleta mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi. Mkutano huo umefanyika kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani.

Mwezi Desemba mwaka 2023, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ilizichagua Tanzania na Philippines, kama wabia wake katika kuandaa programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Bodi hiyo ya MCC ilichukua uamuzi huo baada ya Tanzania na Philippines, kuonesha dhamira mpya ya kusukuma mbele mageuzi muhimu ya kuimarisha utawala wa kidemokrasia, kulinda haki za binadamu na kupambana na rushwa.

Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ni shirika huru la Serikali ya Marekani linalojielekeza kupunguza umaskini duniani kupitia ukuaji wa kiuchumi, kwa kutoa ruzuku na misaada ya muda maalum kwa nchi zinazokidhi viwango na vigezo thabiti vya utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na kuheshimu haki za kidemokrasia.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kulia), akiagana na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden, baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington DC, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea jijini nchini Marekani, ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kupitia Mradi wa Changamoto za Milenia (COMPACT I) uliotekelezwa nchini Tanzania kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2008 hadi 2013, uliiwezesha Tanzania kupata dola za Marekani milioni 698, zilizotumika kutekeleza miradi katika sekta za usafirishaji, nishati na maji.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Washington D.C, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani, ambapo walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga kufanya mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Tunduma – Sumbawanga, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia, Ujezi wa barabara za Pemba, Tanga hadi Horohoro, Ukanda wa Mtwara, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya usambazaji umeme ukiwemo Mradi wa Umeme Jua mkoani Kigoma pamoja kuyajengea uwezo mashirika ya umeme (TANESCO na ZECO).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa nne kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Alice Albright (wa sita kulia), Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC), Bi. Chidi Blyeden (wa tano kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Dkt. Juma Malik Akil (wa nne kushoto), Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (wa kwanza kulia), Mratibu wa Tanzania wa Mradi wa MCC Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kulia), Kiongozi wa Timu ya MCC nchini Tanzania Bw. Nilan Fernando (kushoto), Kamishna wa Idara Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade na Makamu wa Rais wa MCC anayeshughulikia Sera na ukaguzi, Bi. Alicia Mandaville, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao uliofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Washington D.C, ambapo walijadiliana ushirikiano wa shirika hilo na Tanzania katika programu za awali (threshold programs) zitakazolenga katika mageuzi ya kisera na kitaasisi ili kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi, kando ya mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani.

Mradi mingine ni upanuzi wa mtambo wa kusukuma maji wa Ruvu Chini ulioongeza kiwango cha uzalishaji maji kutoka lita milioni 180 hadi lita milioni 270 kwa siku na mradi wa usambazaji maji wa mjini Morogoro ambao uliongeza kiwango cha uzalishaji maji kutoka lita milioni 18 hadi milioni 33 kwa siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news