Dkt.Yonazi ateta na uongozi wa TECDEN

DODOMA-Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Bi. Mwajuma Kibwana (kushoto) pamoja na Bi. Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 07 Mei, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN),Bi. Mwajuma Kibwana (kushoto) walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.Kulia ni Bi. Merina Maneno Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Bi. Merina Maneno, Afisa Utawala wa Taasisi ya TECDEN walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Tanzania ECD Network (TECDEN) Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 07 Mei, 2024.Kushoto ni Mkurudenzi Mtendaji wa TECDEN Bi.Mwajuma Kibwana na wa kwanza kulia ni Bi. Merina Maneno.

Dkt. Yonazi amekutana na uongozi huo Mei 7, 2024 ambapo walijadili kuhusu kazi za Taasisi hiyo ikiwemo ya uratibu wa Mashirika na Wadau wasio wa Kiserikali katika masuala mazima ya malezi, makuzi ya awali ya watoto wadogo kuanzia umri 0 hadi miaka 8.

Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau ikiwemo Taasisi hiyo ili kuendelea kuleta matokeo yenye tija kwa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news