ARUSHA-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo tarehe 10 Mei, 2025 amefanya ziara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwepo mradi wa Ujenzi wa Jengo la kisasa la Makumbusho ya Jiolojia, Ujenzi wa Jengo la Makao makuu ya NCAA linalojengwa nje ya Hifadhi ya Ngorongoro katika Wilaya ya Karatu.