Mrisho Gambo achomoa nati,asema amechoka kuchokonolewa

ARUSHA-Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini mkoani Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo anaonekana kuchoka kwa kile ambacho anasema ni masimango ambayo hayana nyuma wala mbele yanayomuhusu yeye binafsi na nafasi ya uongozi aliyonayo.

"Kuna mambo mengine sikutaka kuyasema kwa sababu nina uwezo mkubwa sana wa kupuuza, lakini nimechokonolewa sana na baadhi ya watu kiasi ambacho inawezekana kuna baadhi ya watu mkachanganywa.

"Kwa hiyo kwa sababu nimelazimishwa, mengi nitapuuza, nitasema walau moja, naomba mnikubalie.Kuna mtu mmoja ambaye amekuwa akijinadi siku nyingi anasema wakati anaenda kwenye SendOff alitumia Koti langu mimi mtoto wa muuza uji.
"Lakini leo hii anadiriki kufikia kusimama mahali anasema eti Gambo ameumiza watu wengi, leo nataka niwaulize hivi mimi na yeye nani ameumiza watu wengi katika nchi hii? Hivi mnapajua Dar es Salaam ninyi? Nendeni mkatafute habari zake kule hata kumsalimia mtaogopa.

"Nataka popote alipo mumuambie mikono yangu ni safi,sina changamoto yoyote na sijamuumiza yeyote badala yake nimesaidia watu wengi sana kote nilipopita.

"Nimesaidia watu wenye ulemavu, tumewapatia viti mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia, tumewasaidia watu kupata miguu bandia ambao hawakutarajia kupata ulemavu, tumesaidia vituo vya yatima, tumesaidia kila mahali. Mwambieni hayo ni matendo mema hakuna hata moja la kumuumiza mtu.

"Na nimeamua nisema kwa sababu amesema eti nenda kwa wananchi wa Arusha, nenda kawaombe radhi, wananchi wa Arusha nimewahi kuwakosea?."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news