Robert Prevost (Papa Leo XIV) ndiye Papa mpya wa Kanisa Katoliki Duniani

VATICAN-Kardinali Robert Prevost kutoka nchini Marekani amechaguliwa kuwa Papa wa 267 wa Kanisa Katoliki Duniani ambapo muda mfupi baada ya moshi mweupe kufuka juu ya Kanisa la Sistine Chapel alifichua cheo chake kipya, Papa Leo XIV.
Franco Origlia/Getty Images.

Papa mteule anachukua nafasi ya Papa Francis ambaye alifariki hivi karibuni akitokea Amerika  Kusini.

Uchaguzi wa papa huyo umefanyika kupitia kongamano la makadinali ambalo lilikuwa likifanyika kwa usiri mkubwa mjini Vatican.

Prevost ndiye Papa wa kwanza wa Amerika katika historia ambapo taarifa za uchaguzi huo zimetolewa na Kadinali Dominique Mamberti wa Ufaransa.

Aidha, Papa huyo akiwa na umri wa miaka 69 anatoka Chicago nchini Marekani. CNN imeripoti kwamba, Prevost alifanya kazi ya umishonari nchini Peru na aliongoza ofisi ya Vatikani ya kuwachunguza maaskofu.Pia, alikuwa Askofu wa Chiclayo kuanzia mwaka 2014 hadi 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news