Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza Johari aapishwa kuwa Mbunge

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Mbunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa kumi na tatu(13) wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kwa mujibu wa Ibara ya 59(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa mamlaka ya kuwa Mbunge na kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha,uapisho huo mbele ya Bunge wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, unafuatia Uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kumteua Mhe. Hamza S. Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali mnamo tarehe 3 Novemba, 2025 na kufuatiwa na uapisho uliofanyika tarehe 5 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here