Amani ya Tanzania haina mbadala,kila mmoja awajibike kuilinda

DODOMA-Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa wito kwa kila mwananchi kuendelea kutii sheria sambamba na kushirikiana na kila mmoja kwa nafasi yake katika kulinda na kuimarisha amani, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa amani katika maisha na shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania,Naibu Kamishna wa Polisi, DCP David Misime, amesisitiza kupitia taarifa yake kwa umma kuwa, kila mmoja kuendelea kuelimishana na kuhimizana katika kuyakataa yale yote yanayohamasishwa kwa njia mbalimbali ili kuwachonganisha na kuwajengea chuki Watanzania.

Lengo likiwa ni kuwaingiza Watanzania katika vurugu ambazo mara zote zimekuwa si nzuri kulingana na kile kinachoshuhudiwa kwenye Mataifa mengine duniani.

"Jeshi la Polisi pia kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vinaendelea kuwaahidi kuwa tutaendelea kulinda usalama wa nchi yetu sote, maisha na mali za kila mmoja ndani ya Taifa letu la Tanzania," ameeleza DCP Misime.

Vilevile, jeshi hilo limeeleza kuwa,nchi bado ni salama na shughuli za kiuchumi na za kijamii zinaendelea vyema katika kipindi cha saa 24 zilizopita, likishukuru pia kwa ushirikiano wanaoendelea kuupata kutoka kwa Watanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here